Afrika Kusini kuanza kulegeza vizuizi vya kupambana na corona

Afrika Kusini itaanza kuondoa vizuizi vyake vya kupambana na virusi vya corona mwishoni mwa mwezi huu. Rais Cyril Ramaphosa ameyasema hayo jana wakati akilenga kuweka usawa kati ya kuwalinda watu na kuwaruhusu wajitafutie kipato.

Rais amewahimiza watu kuvaa maski wanapokuwa nje na kuonya kuwa watu wataruhusiwa tu kukusanyika katika vikundi vidogo kwa ajili ya mazishi na kazi.

Ramaphosa pia amesema mipaka ya nchi hiyo itaendelea kufungwa. Watu milioni 58 nchini Afrika Kusini wamefungiwa majumbani mwao kwa wiki tano, isipokuwa tu kama ni kununua chakula au dawa. Nchi hiyo imerekodi visa 3,953 vya maambukizi na vifo 75.

Vikosi vya usalama viliwauwa raia kadhaa kuhusiana na madai ya kukiuka hatua za kufungwa shughuli nchini humo, ikiwa ni pamoja na marufuku kamili ya biashara ya pombe.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items