Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson anapanga kurejea kazini Jumatatu wiki ijayo ili kuchukua udhibiti wa mgogoro wa virusi vya corona.
Hayo ni kwa mujibu wa ripoti ya gazeti la Uingereza la Daily Telegraph.
Mapema mwezi huu, Johnson aliruhusiwa kuondoka hospitali moja ya London na amekuwa akiendelea kupata nafuu kutokana na ugonjwa wa COVID-19 katika makazi yake ya Chequers.
Johnson anakabiliwa na ukosoaji kutoka kwa wanasiasa wa upinzani na baadhi ya watalaamu wa maradhi ya mlipuko kwa kuchelewa kuanzisha juhudi za kupambana na virusi vya corona.
Uingereza inakaribia kilelele cha mgogoro wa kiafya huku idadi ya vifo kutokana na virusi vya corona ikifika watu 18,738, ikiwa ni taifa la tano ulimwenguni lenye idadi kubwa ya vifo.