Avaa nguo za polisi na kuua watu 10 Canada

Watu wasiopungua 10 wameshambuliwa kwa risasi na kuuawa na mtu aliyevaa mavazi ya afisa polisi Nova Scotia nchini Canada.

Mmoja wa waliofariki ni afisa polisi huku mwingine mmoja akiwa amejeruhiwa, Hakuna taarifa kamili iliyotolewa kuhusu wale waliopoteza maisha lakini shambulizi hilo limetokea katika maeneo tofauti ya Nova Scotia.

Mshambuliaji huyo baadaye alipigwa risasi na polisi na kuuawa, Kulingana na vyombo vya habari nchini Canada,mauaji hayo yalianza saa chache kabla ya usiku wa manane Jumamosi na yakaendelea hadi Jumapili wakati mtuhumiwa, Gabriel Wortman, 51, alipovaa mavazi ya polisi  na kuendesha gari lililofanana na gari la polisi na kisha kuingia katika eneo la Nova Scotia kwa ajili ya kuanza mashambulizi.

Mashambulizi yalianza katika kijiji kidogo cha Portapique, Nova Scotia,kijiji chenye watu karibu 300 na ambapo mtuhumiwa huyo alikuwa akiishi.

Polisi wamethibitisha kuwa watu angalau 10 wamepoteza maisha.Hata hivyo uchunguzi wa maeneo yote yaliyoshambuliwa haujakamilika.

Katika mkutano na waandishi wa habari, Waziri Mkuu Justin Trudeau pia amezungumza kuhusiana na tukio hilo na kuonyesha masikitiko makubwa.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items