Wanazuoni wa kiislamu watoa tamko kuhusu ibada ya funga la Ramadhani katika kipindi cha janga la corona.
Wanazuoni wa kiislamu watoa tamko kuhusu ibada ya funga ya mwezi mtukufu wa Rmadhani katika kipindi ambacho ulimwengu mzima umekumbwa na janga la virusi vya corona, virusi ambavyo tayari vimesababisha maafa makubwa ulimwenguni.
Wanazuoni hao wamefahamisha kuwa janga la virusi vya corona halina athari yeyote kwa watu ambao hawana maradhi ya aina yeyote, wakimaanisha kuwa mtu ambae ni mzima wa afya atalazimika kudiriki ibada hiyo ya funga ispokuwa kwa wale ambao watakuwa wameathirika na hiyo ni chini ya misingi ya uislamu.
Uislamu imeweka wazi watu ambao wanalazimika kufunga na wale ambao hawalazikimi kufunga kama wagonjwa.
Muungano wa wanazuoni mwa kiislamu umefahamisha kuwa virusi vya corona havimzuia kufunga Radhani muislamu ambae afya yake ni salama.
Tamko hilo limetolewa baada ya uvumi na maswali mengi kujitokeza katika jamii kuhusu ibada ya funga katika mwezi mtukufu wa Ramadhani ambao umewadia.