Barakoa zawa ‘deal’ jiji la Dodoma

KUTOKANA na kuwepo kwa mahitaji ya matumizi ya barakoa kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona kifaa hicho kimekuwa lulu katika jiji la Dodoma.

Hali hiyo imetokana na serikali kutoa maelekezo ya kuvaa barakoa kwa ajili ya kujilinda na virusi hivyo na wananchi kuwa na mwamko wa kuelewa na kujali matumizi ya barakoa.

Hali hiyo imeonekana baada ya uchunguzi na utafiti wa gazeti hili na kubaini kuwa barakoa kuwa hadimu katika maduka mengi ambayo yanauza madawa ya binadamu pamoja na vifaa tiba.

Kitendo cha barakoa kuwa adimu katika maduka halali ya kuuza madawa baridi ya binadamu imepelekea mafundi chelehani kuanza kufanya biashara ya kushona barakoa na kuanza kuzitembea mitaani.

Katika kuthibitisha kuwepo kwa uhaba wa barakoa madukani, Meneja wa duka la Nakiete Jijini Dodoma, Attilio Elia, alisema suala la barakoa limekuwa changamoto kubwa katika upatikanaji wake hasa tangu serikali kutoa maelekezo ya kuwepo kwa matumizi ya barakoa.

Alisema kuwa baada ya serikali kutilia mkazo wa utumiaji wa barakoa, Nakiete imekuwa msitari wa mbele katika kutafuta barakoa ambazo zipo katika viwango ambavyo vinatakiwa kwa mujibu wa sheria ya viwango kwa ajili ya kuwapatia wateja wao.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items