COVID-19 inaongeza kitisho cha uhuru wa habari duniani


Shirika la kutetea haki za waandishi habari la Maripota Wasio na Mipaka limetahadharisha kuwa jkanga la virusi vya corona linaweka kitisho kikibwa kwa uhuru wa waandishi habari kote duniani.

 Katika tathmini yake ya kila mwaka ya uhuru wa habari duniani, shirika hilo limeonya leo kuwa mgogoro wa sasa wa kiafya huenda ukatumika kama kisingizio kwa serikali kutumia fursa ya ukweli kwamba siasa zimesitishwa kwa muda, umma umepatwa na mshtuko na maandamano hayapo tena kwa sasa, ili kuweka hatua ambazo hazingewezekana katika nyakati za kawaida

Korea Kaskazini imeorodheshwa katika nafasi ya mwisho ya faharasa ya viwango vya uhuru duniani. Kama tu mwaka wa 2019, Norway imeongoza tena orodha hiyo ya nchi 180.
Mpya zaidi Nzee zaidi