Jeshi lawashambulia magaidi nchini Nigeria


Jeshi la Nigeria limewaua magaidi wasiopungua 105 wiki iliyopita katika harakati za kukabiliana na kundi la Boko Haram.

Msemaji wa Jeshi la Kanali, Sagir Musa amewaambia waandishi wa habari kwamba magaidi hao waliuawa katika jimbo la kaskazini mashariki mwa Yobe nje kidogo ya kijiji cha Buni Gari.

Musa ameendelea kwa kusema kuwa askari wawili wamejeruhiwa katika harakati za kuwaangamiza magaidi hao na kwamba silaha nyingi za magaidi zimekamatwa.

Kundi la Boko Haram limekua likifanya mashambulizi na kumwaga damu nchini Nigeria tangu mwaka 2009.

Kundi hilo lilianzia kaskazini mashariki mwa Nigeria a baadaye kuendeleza ugaidi wake katika nchi kama Niger,Chad na Cameroon.

Kulingana na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Uratibu wa Masuala ya kibinadamu,zaidi ya watu 30,000 wameuawa na karibu milioni 3 wameyahama makazi yao katika muongo mmoja wa mashambulizi ya kigaidi za Boko Haram nchini Nigeria.

Vurugu zinazosababishwa na Boko Haram zimeathiri watu wapatao milioni 26 katika eneo la Ziwa Chad na kuwahamishamakazi wengine milioni 2.6.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items