Kanisa la Anglikana Dodoma laongeza idadi ya ibada kupunguza misongamano

Ikiwa ni kupunguza misongamano katika Ibada kanisa la Anglikana Dayosisi ya Central Tanganyika imeamua kuongeza idadi ya Ibada ili kupunguza msongamano katika kuwakinga waumini wao dhidi ya maambukizi ya virus vya Corona.

Pia wamepongeza uamuzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt John Magufuli kwa kutozuia Ibada kuendelea nchi nzima ili kuweza kuliombea taifa ili Mungu atuepushe na janga la kuenea kwa virus vya Corona.

Akizungumza Mara baada ya kumalizika kwa Ibada ya kwanza ya jumapili ya mitende Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Central Tanganyika Dodoma, Dkt Dickson Chilongola, amesema kwa kauli moja wamekubaliana kuongeza idadi ya ibada kutoka ibada tatu (3) hadi nne (4).


"Tumekubaliana kuwa kutokana na janga hili Sasa tunaongeza idadi ya ibada Sasa zitakuwa nne ya kwanza itaanza saa kumi na mbili  kamili asubuhi na kumalizika saa moja na robo, ya pili inaanza saa moja na nusu na kumalizika saa tatu , na tatu kuanza saa tatu na robo mpaka saa tano na ya mwisho itakuwa saa tano mpaka saa saba mchana" amesema Askofu Dkt  Chilongola.

Aidha amepongeza uamuzi wa Rais wa kutofuta Ibada na kusema ni uamuzi wa kijasili na ambao hutolewa na watu wenye kumcha Mungu, huku akisema uamuzi wa kuliombea taifa huku ibada zikiendelea ni mzuri.

Aidha amebainisha kuwa sambamba na kuendelea na ibada wamekuwa wakifuata njia zote zinazoshauriwa na wataalamu wa afya za kujikinga na ugonjwa huo ili usienee zaidi.

Kwa upande wake Katibu wa Kanisa hilo bwana Chrisper Mlale amesema yeye Kama mtendaji Mkuu wa Kanisa anahakikisha vifaa vyote vinapatikana kila pembe ya kanisa hilo ili kila mtu aweze kujikinga.

" Sisi hapa tunahakikisha kila muumini anayeingia kanisani anakuwa amenawa kwa maji wenye dawa, na kila ibada inapoisha tunahakikisha mabenchi na viti vyote vinapuliziwa dawa ya kuua vimelea vya aina yoyote" amesema Mlale.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items