Marekani yataka Afghanistan ipunguziwe msaada

Marekani hii leo imeishauri Jumuiya ya Kimataifa kusitisha msaada kwa Afghanistan hadi viongozi wa nchi hiyo watakapoamua kuhusu serikali ya pamoja.

Mwanadiplomasia wa wizara ya mambo ya kigeni ya Marekani anayeshughulikia eneo la Asia Kusini na Kati Alice Wells aliandika katika mtandao wake wa twitter kwamba, usaidizi wa kimataifa unahitaji ushirikiano na serikali ya pamoja inayojumuisha kila mtu, na kwamba kila mmoja anapaswa kuhakikisha viongozi wa Afghanistan wanakubaliana kuhusu namna watakavyiongoza nchi.

Mwezi uliopita Marekani ilitangaza punguzo la dola bilioni moja za msaada wake nchini Afghanistan baada ya rais Ashraf Ghani na mpinzani wake afisa mkuu mtendaji Abdullah Abdullah kushindwa kuunda serikali kufuatia matokeo ya uchaguzi uliokabiliwa na utata.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items