Waziri wa afya wa Uingereza Matt Hancock amekanusha kuwepo kwa aina yoyote ya kutokukubaliana na waziri wa fedha Rishi Sunak kuhusu wakati ambapo vizuizi vya kubakia nyumbani ili kupambana na virusi vya corona vitakapoondolewa.
Gazeti la Uingereza limeripoti Sunak amekuwa akisisitiza kuainishwa maeneo yatakayoondolewa vizuizi hivyo ili kusaidia kupunguza hasara za kiuchumi.
Lakini Hancock amenukuliwa akisema wanafanya kazi pamoja kuhakikisha wanaondoka katika janga hilo haraka iwezekanavyo.
Amesema wanataka kuhakikisha watu wengi wanafuata maagizo ili kupunguza kusambaa kwa virusi vya corona.
Wakati huohuo malkia Elizabeth wa pili wa Uingereza anatarajiwa kulihutubia taifa leo jioni.
Hotuba yake itaperushwa moja kwa moja kupitia televisheni ya kitaifa nchini humo hii ikiwa ni kwa mujibu wa kasri la Buckingham.
Hotuba yake itaangazia mikakati ya Uingereza kudhibiti virusi vya corona.