Makampuni ya mabasi wamtaka waziri kuingilia kati mzozo wao na halmashauri ya Jiji la Tanga



Na Rebeca Duwe, Tanga.

Wamiliki wa kampuni za mabasi ya Tawakal na Simba Mtoto za Jijini Tanga, wamemuomba Waziri wa Uchukuzi kuingilia kati mzozo wao na halmashauri ya Jiji la Tanga ya kuwazuia wasibebe abiria katika maeneo yao maalum ya kupakia abiria 'Terminal'.

Hayo wameyasema  wakati wakiongea na waandishi wa habari walisema kuwa wamesikitishwa na kitendo cha Halmashauri kuwapiga marufuku kutumia terminal zao kwa ajili ya kushusha na kupakia abiria.

Meneja wa kampuni ya Tawakal Athuman Athuman Abdulrahman alisema kuwa kutokana na kituo cha mabasi ya Kange kukosa huduma muhimu imekuwa ni kikwazo kwa wateja wao kupata huduma bora.

''Tunaomba wizara itusaidie katika hili kwani kampuni yetu inahudumia wateja kutoka nje ya nchini sasa akiingia nchini anakutana na kituo ambacho hakina huduma muhimu na hivyo huwa ni kero kwao'alisema Athuman.

Aidha alisema kuwa licha ya kufanya ukarabati mkubwa katika eneo lao lakini wanashangazwa na kitendo cha Halimashauri kuweka zuio la wateja wao kupakia katika ofisi zao na badala yake abiria wote watumie kituo cha kange.

Kwa upande wake meneja wa kampuni ya simba mtoto Mohammed Said alisema ipo haja ya serikali kuingilia kati suala hilo kwani wao wamiliki wa magari wamekuwa na mchango mkubwa sana kwa Taifa hususani katika ulipaji kodi.

Alisema suala la wao kuhamishiwa stendi ya kange linawaathiri kwa kiasi kikubwa kutokana na gharama kubwa walizotumia kukarabati vituo vilivyopo mjini kwajili ya kuhudumia wateja wao.

''Mwanzoni tulikubaliwa tufanye maboresho ya maeneo yetu lakini mara baada ya kukamilika ndio tukaambiwa huduma zote tukazifanyie standi kuu ikiwa tayari tumeshatumia gharama kubwa kufanya maboresho katika maeneo yetu,''alisistiza Mohammed.

Sambamaba na hayo wamiliki hao walisema wanashangazwa kitendo cha kuambiwa wahamie standi ya Kange ambayo  ina msongamano wa watu ikiwa hivi sasa mataifa mbalimbali yanakabiliana wa ugonjwa wa Covid 19.

''Nashindwa kuelewa kwanini wanafanya maamuzi haya sizani kama kuna sababu ya kutuondoa katika terminal zetu kiukweli hatujui wametumia vigezo gani kutuondoa isitoshe kange kuna msongamano wa watu ni tofauti na huku kwenye terminal zetu watu wako kwenye usalama zaidi.

Akijibu malalamiko hayo mkuu wa mkoa wa Tanga Martin Shigela Alisema kwa sasa hawezi kulizungumzia suala Hilo nakwamba utaratibu unafahamika kwa wamiliki wote wa mabasi " Kwasasa siwezi kulizungumzia suala hili Mana tupo kwenye mapambano  dhidi ya Corona lakini utaratibu unafahamika kwa wamiliki wote wa mabasi" alisisitiza Shigela.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items