Na Rebeca Duwe, Tanga.
Mkuu wa mkoa wa Tanga Martin Shigela , asisitiza maagizo ya Rais Dkt.John Pombe Magufuli kwa wakazi wa mkoa huo , ya kuendelea kuzingatia maagizo ya serikali ikiwa ni pamoja na kutumia Dawa za asili ambazo huwa wanazitumia kwa ajili matatizo ya mafua kawaida ambayo pia inapatikana kwa urahisi.
Hayo ameyasema wakati akipokea masaada wa kiasi cha sh. Milioni 10 kutoka kwa kampuni ya JIANGXI GEO-ENGINEERING(GROUP)CORPORATION ya kichina ambayo amekabidhiwa na Mkurugenzi wa kampuni hiyo GM Mr. Chen Xianghuu ambapo amesema ni kwa ajili ya kuunga mkono shughuli za Serikali za kupambana na maambukizi ya Ugonjwa wa Corona ulioathiri ulimwengu pamoja na Tanzania kwa ujumla.
Shigela amasema kwamba Mkoa wa Tanga una misitu mingi na hivyo zipo Dawa za asili zipo zingine zilizosajiliwa za zisizosajiliwa inayotokana na miti ambapo ni Tangawizi , Binzari , limau na vitunguu saumu laikini pia kuzingati kukaa umbali wa mita moja kutoka mwingine hadi mwingine.
Alisema kwamba wananchi wanaofanya biashara wakiwemo wale wanaofanya mshughuli za baa, kuendelea kuzingatia utaratibu uliowekwa wa kuzingatia maagizo ya serikali na kuweza kuwashauri wateja wao kufuata maelekezo yalioweka na serikali ya kutokukumbatiana na kushikana na kwamba endapo itatokea wameshikana wanatakiwa kunawana mikono na sabuni au kutumia vitakasa mikono.
Alisema kuwa hakuna tiba ya ugonjwa Corona isipokuwa ni kuzingatia maagizo ya serikali na wataalamu wa afaya , na kuongeza kusema kuwa pesa hizo walizopokea zitaingizwa kwenye mfuko maalumu wa Covid 19 unaoratibiwa Waziri Mkuu ili kuweza kusaidia kwenye janga la maambukizi ya ugonjwa huo.
Alisema JGC kichina ni kampuni inayojishugulisha na ujenzi hapa Tanzania , ambayo ina miradi mikubwa hapa Tanga imesaidia na kujenga wa Barabarabara, wamejenga barabara ya Makorora, Msambwewni, Standi ya Kange ambayo iko penmbeni ,na kujenga Dambo la kuelkea mtimbwani hivyo wameamua kuunga mkono serikali katika mapambano ya COVID 19.
Kwa upande wake katibu Tawala mkoa Tanga Judica Omari ameishukuru Kampuni hiyo kwa kutoa msaada huo kwani itasaidia katika kupambana na covid 19 kama ambavyo imekusudiwa naserikali kuunda mfuko maalum wa kuwekafedha za maafa ambapo fedha hizo zitaingizwa.
