Virusi vya corona: Rais Macron alishukuru jimbo la Ujerumani


Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amelishukuru jimbo la Ujerumani la North Rhine Westphalia kwa kuwapatia matibabu wagonjwa wa Kifaransa waliopata maambukizi ya virusi vya corona.

Katika barua aliyomtumia waziri mkuu wa jimbo hilo Armin Laschet na kuonekana na shirika la habari la dpa, Macron amesema wale waliopata maambukizi makali ya virusi hivyo waliweza kupewa huduma bora ya matibabu baada ya kusafirishwa nchini Ujerumani.

Mwishoni mwa mwezi Machi, wagonjwa wanane waliokuwa katika hali mbaya walisafirishwa kutoka mji wa Ufaransa wa Metz hadi mji wa Ujerumani wa Essen, ulio karibu na mpaka wa Ufaransa.

 Mgonjwa mmoja aliyekuwa na umri wa miaka 76 alifariki dunia hospitalini Jumatatu iliyopita na wagonjwa wengine wawili walirudishwa Ufaransa baada ya kupata afueni.

Wagonjwa zaidi wataendelea kutibiwa mjini Essen.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items