Naibu Waziri wa Afya Dkt Faustine Ndugulile amesema mask za vitambaa hazimkingi mtu kupata virusi vya Corona, isipokua kuna mask maalum zilizothibitishwa na wataalamu wa afya kulingana na 'material' yaliyotengenezewa ndio zinazuia maambukizi kwakuwa zimewekwa vitu maalumu.
Dkt. Ndugulile ameyasema hayo Bungeni leo wakati akitoa taarifa kwa Bunge, kuhusu matumizi sahihi ya mask na uwepo wa mask za vitambaa mtaani ambazo Mbunge Richard Ndasa aliingia nazo Bungeni kwa lengo la kutaka punguzo la bei la vifaa hivyo ambavyo mtaani vinauzwa bei kubwa.
Wakati huohuo Dkt. Ndugulile amesema ugonjwa wa Covid 19, mtu akipata maambukizi ni kazi ya mikono yake kwakuwa ugonjwa huo huambukizwa pindi mtu anaposhika majimaji ya mgonjwa wa Covid 19 na sio kwa njia ya hewa kama wengi wanavyodhania.