Rais wa Brazil aungana na waandamanaji kupinga amri ya kubakia nyumbani


Rais Jair Bolsonaro wa Brazil jana alijiunga na takribani waandamanaji 600 nje ya makao makuu ya jeshi kupinga amri ya kubakia nyumbani iliyotangazwa na Magavana wa majimbo ili kujikinga na corona, Rais Jair amesema amejiunga nao kwakuwa anakubaliana na mawazo yao.

Kundi hilo la waandamanaji limetoa wito kwa Jeshi kuingilia kati hatua za kupambana na corona, Rais Bolsonaro mara kadhaa amekosoa hatua zilizochukuliwa na Magavana za kuweka vizuizi vya wastani ikiwemo kwenye miji yenye idadi kubwa ya watu ya Sao Paulo na Rio de Janeiro ili kuzuia kusambaa kwa corona.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items