Mahakama ya juu nchini Saudi Arabia imetangaza kufuta adhabu ya viboko na kusifu hatua hiyo kuwa moja ya mageuzi muhimu katika kulinda haki za binadamu yaliyofanywa na mfalme Salman na mtoto wake wa kiume, mwanamfalme Mohamed.
Mahakama hiyo imesema mageuzi hayo yanalenga kuifanya Saudi Arabia kuwa falme inayoheshimu desturi za kimataifa kuhusu Haki za Binadamu zinazopinga adhabu ya viboko.
Hapo kabla mahakama nchini Saudi Arabia zimekuwa zikitoa adhabu ya viboko kwa watu waliotiwa hatiani kwa makosa ikiwemo kufanya mapenzi nje ya ndoa, kuvuruga amani na hata mauaji.
Kwa muda mrefu amri za mahakama za kuwacharaza wahalifu viboko ambavyo wakati mwingine vilipindua 100 zimekabiliwa na ukosoaji mkubwa kutoka makundi ya kutetea haki za biandamu.
