Vipindi vya masomo kwa TV na Radio

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, imezindua rasmi urushaji wa vipindi vya masomo kupitia televisheni za Channel Ten na Azam, pamoja na redio 34 za kijamii, katika maeneo mbalimbali nchini ili wanafunzi kuanzia ngazi ya awali hadi kidato cha sita waweze kupata masomo wakati huu wa kipindi cha Corona.

Akizindua mpango huo jijini Dodoma, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo, amefafanua kuwa wizara imeandaa vipindi hivyo kupitia Taasisi ya Elimu Tanzania.

Aidha, Katibu Mkuu huyo wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, akafafanua juu ya vipindi vilivyoandaliwa na Baraza la Mitihani la Tanzania, kwa ajili ya madarasa yanayofanya mitihani.

Dkt. Akwilapo, pamoja na kuvishukuru vituo vitakavyorusha vipindi hivyo, pamoja na wadhamini NBC, lakini akawahasa wazazi na walezi kuwafuatilia kwa karibu watoto, ili kuhakikisha wanajifunza kupitia vipindi hivyo.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items