Na Ezekiel Mtonyole, Dodoma.
Baada ya Serikali kutangaza kufungua vyuo vyote na shule kwa kidato cha sita bodi ya mikopo ya elimu ya juu imetoa kiasi cha sh bilioni 63. 83 kwa ajili ya awamu ya tatu ya wanafunzi wa vyuo vikuu hapa nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 29, 2020 Mkurugenzi wa Bodi ya mikopo Abdul Razaq Badru amesema fedha hizo ni kwa ajili ya awamu ya tatu ambao awamu mbili za mwanzo tayari zilishatolewa.
"Sisi kama bodi ya mikopo tayari tumeshatoa fedha kwa ajili ya mikopo kiasi Cha shilingi bil.63.83, ikiwa ni awamu ya tatu baada ya awamu ya pili kukamilika" amesema Badru.
Amesema tayari fedha hizo zimeshapelekwa katika vyuo vyote vyenye sifa na tayari maafisa mikopo wamesha pelekwa vyuoni kwa ajili ya kushughilikia na mikopo ya kuhakikisha wanafunzi wanapata kwa wakati.
Amesema wanafunzi wasiogope warudi vyuoni kuendelea na masomo kwa sababu serikali imejipanga kwa kila kitu na kuwataka kuanza kuripoti kwa ajili ya kujisajili.
"Naomba wanafunzi wasiogope warudi shuleni ili kuendelea na masomo kwa ajili ya kuendelea na masomo, " amesema.
Amebainisha kuwa usajili umeanza leo utaendelea hadi Jumapili lakini watakaochelewa usajili utaendelea Jumatatu.
Amesema wanafunzi waliopo 132, 119 na taasisi zilizopelekewa fedha hadi sasa ni zaidi ya 70 zilizopo hapa nchini.
Amesema malipo ni ya siku 60 ambapo ni kwa ajili ya malazi na chakula ambayo wanafunzi wanaita bumu.
Naye Makamu Mkuu wa chuo kikuu Dodoma UDOM Prof.Faustine Bee amesema chuo kimezingatia suala zima la Corona ambapo wanafunzi watakuwa na Barakoa na vitakasa mikono kwa ajili ya kuendelea kujikinga na ugonjwa huo.
Amesema chuo kina vitakasa Mikono na maji tiririka ambayo watayatumia kwa ajili ya kujilinda na Corona.
Naye Rais wa TAHIRISO, Peter Mboye amesema wanafunzi wajitokeze Vyuoni wakasome kwa bidii ili wahitimu masomo yao katika awamu iliobaki.
Aidha wameishukuru Serikali kutokana na fedha ilizotoa na kusema wao kama wanavyuo ataendelea kuweka jitihada ili kuhitimu masomo yao.
