Na Ahmad Mmow, Lindi.
Taasisi ya Kuzuia na Kupambanana Rushwa( TAKUKURU) mkoani Lindi imefanikiwa kukusanya shilingi 30,000,000 kati ya shilingi 187,000,000 zinazotakiwa kulipwa kwa mamlaka ya mapato( TRA) ikiwa ni kodi ya mapato ambayo inatakiwa kulipwa na chama kikuu cha ushirika Cha Lindi Mwambao.
Leo akizungumza katika ofisi za mamlaka ya mapato( TRA) ya mkoa wa Lindi, mjini Lindi wakati anakabidhi hati ya benki ya malipo ya fedha( slipu)kwa mkuu wa wilaya ya Lindi. Mkuu wa TAKUKURU wa mkoa wa Lindi, Steven Chami alisema kupatikana kwa fedha hizo ni matokeo ya utekelezaji wa agizo la Rais Dkt John Magufuli kupitia kwa waziri wa kilimo na ushirika ambalo alitoa mwaka jana.
Chami alisema baada ya mheshimiwa Rais kuitaka TAKUKURU ichunguze na ifuatilie mwenendo wa ulipaji wa kodi ya mapato unaofanywa na vyama vikuu vya ushirika ilianza kuchunguza vyama vikuu vya ushirika vya RUNALI na Lindi Mwambao ambavyo vipo katika mkoa wa Lindi.
Alisema katika uchunguzi huo ilibaini kwamba chama kikuu cha Mwambao kilikuwa kinatakiwa kulipa shilingi 187,000,000 ambazo zinatokana na kodi ya kipindi cha miaka mitatu.
Mkuu huyo wa TAKUKURU wa mkoa wa Lindi alibainisha kwamba kiasi hicho Cha fedha kilicholipwa ni sehemu ya shilingi 187.00 milioni ambazo zinatakiwa zilipwe na chama hicho kwa TRA.
" Kwabahati nzuri wamekubali kulipa. Bali wamesema hawana kiasi chote cha fedha wanazodaiwa, kwahiyo wamehadi kulipa kiasi kilichobaki. Nasisi ndicho tunachotaka, wanatakiwa walipe fedha zote wanazodaiwa," alisema Chami.
Nae mkuu wa wilaya ya Lindi, Shaibu Ndemanga licha ya kushukuru na kuipongeza TAKUKURU kwa jitihada zilizofanikisha kupatikana fedha hizo, alitoa wito kwa watu wote wanaotambua wanastahili kulipa kodi, walipe bila kusubiri kulazimishwa.
Alisema nchi haiwezi kutekeleza mipango ya maendeleo na kutoa huduma bora kwa wananchi iwapo wanaostahili kulipa kodi wanakwepa na kushindwa kulipa. Kwahiyo kila anayestahili kulipa nilazima alipe, hasa ikizingatiwa kwamba nchi ipo kwenye mkakati wa kujitegemea badala ya kutegemea misaada ya wahisani.
Kwaupande wake meneja wa TRA wa mkoa wa Lindi, Nicodemus Mwakilembe alitoa wito kwa wananchi watoe ushirikiano na mamlaka hiyo kuhusu kodi. Kwani kazi ya kukusanya kodi sio ya TRA peke yake, bali ya wadau wote wa maendeleo. Wakiwamo wananchi.
Alisema hata kiasi hicho cha fedha kilichopatikana kimetokana na jitihada na ushirikiano mkubwa wa wadau, hasa TAKUKURU.