China yadai ni mapema mno kuchunguza shina la kirusi cha Corona

Wizara ya mambo ya nje ya China imesema ni mapema mno kuanzisha mara moja uchunguzi kuhusu kilikoanzia kirusi cha corona pamoja na kusambaa kwake.

Msemaji wa wizara hiyo Zhao Lijian amewaambia waandishi habari wakati wa utoaji wa taarifa za kila siku kwamba nchi nyingi duniani zinaamini kwamba janga la mripuko wa kirusi hicho halijamalizika.

Kufikia sasa zaidi ya watu 300,000 wamekufa duniani kutokana na kirusi hicho.

Wizara hiyo ya mambo ya nje ya China imefahamisha pia kwenye taarifa nyingine kwamba Rais Xi Jinping atatoa hotuba kwa njia ya video ya ufunguzi wa kikao cha baraza la shirika la afya duniani, WHO baadae leo.

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items