Serikali ya Yemen inayoungwa mkono na Saudi Arabia imewashutumu mahasimu wake waasi wa kihouthi kwa kuficha mripuko wa kirusi cha corona katika maeneo wanayoyashikilia.
Serikali iliyoko mjini Aden pia imeomba msaada wa dharura wa jumuia ya kimataifa kuisadia sekta ya afya ya taifa hilo lililokumbwa na vita ili iweze kupambana na janga la kirusi hicho hatari.
Na Umoja wa Mataifa umeonya kwamba nchi hiyo huenda ikatumbukia kwenye janga kubwa la ukosefu wa chakula kutokana na mripuko huo wa kirusi cha corona.
Serikali imeripoti visa 128 vya maambukizi na vifo 20 vinavyofungamanisha na kirusi cha corona kutoka mikoa tisa kati ya 21 ya taifa hilo. Waziri wa serikali za mitaa, Abdul Raqib amewaambia waandishi habari jana kwamba ripoti zinaonesha kuna idadi kubwa ya maambukizi katika maeneo yanaayodhibitiwa na Wahouthi.
Shirika la Afya Duniani, WHO limesema kirusi hicho kinasambaa bila ya kutambulika miongoni mwa watu wa taifa hilo, lililogawika baina ya Kusini ambako inapatikana serikali na upande wa Kaskazini waliko waasi Wakihouthi wanaoegemea upande wa Iran.