Wanaharakati wa demokrasia mjini Hong Kong, wamesema China imeanzisha mashambulizi yake makali zaidi dhidi ya uhuru wa mji huo, kwa hatua yake ya kulaazimisha sheria ya usalama, wakiapa kuingia mitaani kupinga hatua hiyo.
Sheria inayopendekezwa, ambayo inatarajiwa kupiga marufuku uhaini, mapinduzi na uchochezi wa uhaini, iliwasilishwa kwenye bunge la China mwanzoni wa kikao chake cha kila mwaka leo asubuhi.
Hatua hiyo imefuatia onyo ambalo limekuwa likitolewa mara kwa mara kutoka kwa viongozi wa kikomunisti wa China kwamba hawatavumilia tena uasi mjini Hong Kong, mji wenye mamlaka yake ya ndani ambao mwaka uliopita, ulikumbwa maandamano makubwa ya kuteteta demokrasia yaliodumu kwa miezi saba.
Mwanaharakati marufu wa demokrasia Joshua Wong amesema ujuembe wa China kwa waandamanaji ulikuwa wazi, na kuongeza kuwa Beijing inajaribu kunyamazisha sauti za ukosoaji za wa Hong Kong kwa kutumia nguvu na hofu.