Corona: Idadi ya Wagonjwa wa corona kenya yafikia 887

Idadi ya wagonjwa wa virusi vya corona nchini Kenya imeongezeka hadi kufikia 887 baada ya wagonjwa wengine 57 kukutwa na virusi hivyo katika kipindi cha saa 24 zilizopita.

Wagonjwa hao ni wanawake 23 na wanaume 34 wote wakiwa kati ya umri wa miaka miwili na 61.

Katika taarifa iliotolewa na wizara ya Afya siku ya Jumapili, Msemaji wa serikali Cyrus Oguna alisema kwamba kati ya wagonjwa hao wapya mjini Mombasa , Nairobi 17 , kajiado 3 huku Kwale na Kitui zikitangaza wagonjwa mmoja mmoja mtawalia.

Wagonjwa hao wapya walipatikana baada ya smapuli 2198 zilzipimwa, Kufikia sasa taifa hilo limefanikiwa kupima watu 43,712.

Katika taarifa iliotolewa na kanali mstaafu Oguna amesema kwamba wagonjwa 35 wanatoka Mombasa, huku 22 wakitoka Mvita ina wagonjwa 2 likoni wanne huku Changamwe na Nyali zikiwa na wagonjwa watatu kila moja.

Kisauni ina wagonjwa wawili huku Jomvu ikitangazaa mgonjwa mmoja.

Mjini Nairobi , Kibra ilikuwa na wagonjwa tisa katika kituo cha kujitenga cha serikali, Eastleigh ikiwa na wagonjwa 2 huku hospitali ya Aga Khan, Kamulu, Dandora na Pangani zikiwa na mgonjwa mmoja kila mmoja.

Amesema kwamba madereva wengine 12 wa malori ya kubeba mizigo kutoka Tanzania walikutwa na virusi hivyo.

Amewataka Wakenya kufuata muongozo wa Kiafya ili kuzuia kusambaa virusi hivyo.

''Idadi ya leo ya wagonjwa inaonesha wazi kwamba ugonjwa huo bado upo ndani yetu na kwamba maambukizi bado hayajapungua. Hivyo basi tunatoa wito kwa Wakenya kuendelea kufuata maagizo ya kuwalinda dhidi ya ugonjwa huo'', alisema.

Kwa habari njema, serikali imesema kwamba watu 12 waliruhusiwa kuondoka hospitalini , na hivyo basi kufanya idadi ya waliopona kufikia 313.