Mfumo wa kuwafuatilia wanamgambo Pakistan kutumika kuwafuatilia wagonjwa wa COVID-19


Idara ya ujasusi ya Pakistan imeanza kutumia teknolojia ya siri ya uchunguzi ambayo awali ilitumika kuwafuatilia wanamgambo na badala yake hivi sasa itatumika kuwafuatilia wagonjwa wa COVID-19 na watu waliokaribiana nao. 

Chini ya programu hiyo ambayo ilitangazwa hadharani na waziri mkuu Imarn Khan serikali sasa inaigeukia idara hiyo yenye nguvu, ISI kusaidia kupambana na virusi vya corona ambavyo bado vinasambaa kwa kasi kote nchini humo. 

Hata hivyo bado program hiyo haijaelezewa kwa kina lakini maafisa wawili wameliambia shirika la habari la AFP kwamba, idara ya ujasusi wanatumia mifumo ya kimaeneo na mawasiliano ya simu ambayo awali ilitumika kuwafuatilia wanamgambo wa ndani na wa kutoka nje. 

Kiasi watu 60,000 wameambukizwa virusi hivyo nchini Pakistan wakati kukiwa na maambukizi yanayokaribia milioni 6 kote ulimwenguni.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items