Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amewaonya viongiozi wa dunia kwamba janga la virusi vya corona litasababisha uharibifu mkubwa na mateso ulimwenguni, huku kukiwa na kitisho cha hali ya ukame na njaa kwa takribani watu milioni 1.6, ambao hawana uwezo wa kujikwamua pasipo kuchukuliwa hatua madhubuti.
Akizungumza katika mkutano wa juu hapo jana alisema ugonjwa wa COVID-19 vilevile utasababisha hasara ya dola bilioni 8.5, kwa pato la ulimwengu, kikiwa ni kiwango kikubwa kufikiwa miaka ya 1930.
Kutokana na hali hiyo Guterres ametoa wito wa kufanyika jitihada za pamoja katika kuyashughulikia maeneo muhimu.
