Japan yakumbwa na tetemeko la ardhi

Tetemeko lenye ukubwa wa 5,2 katika kipimo cha Richter nchini Japan.

Tetemeko la ardhi lenye  ukbwa wa 5,2 katika kipimo cha Richter laripotiwa kutokea nchini Japan.

Taarifa hiyo kuhusu tetemeko imetolewa na kitengo cha utafiti wa ardhi  nchini humo.

Kitengo hicho kimesema kwamba tetemeko hilo limetokea katika kisiwa cha Honshu na kusikika  hadi katika umbali wa  kilomita  10 na  eneo la Gifu.

Tetemeko hilo limetokea  saa moja usiku majira ya Honshu.

Taarifa zinasema kuwa hakuna  tishio la wimbi kubwa la Tsunami baada ya tetemeko hilo.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items