Rais Erdoğan akemea mwenendo uliopelekea kifo vya George Floyd nchini Marekani

Rais Recep Tayyıp Erdoğan akemea vikali  kitendo kisichokuwa cha kibinadamu kilichosababisha kifo cha George Floyd.

Rais wa Uturuki Recep Tayyıp Erdoğan amekemea vikali  kitendo cha   kinyama kilichopelekea kifocha mmarekani mweusi George Floyd kwa kukandamizwa kwa goti shingoni hadi kukata roho.

Rais Erdoğan ameuzunishwa na kifo cha mmarekani huyo mweusi mikono mwa maafisa wa usalama ambao ilitakiwa kuwa kimbilio.

Katika ujumbe wake aliotoa kipiti aukurasa wake  katika mtandao wa kijamii wa Twitter, rais Erdoğan   ameonesha msimamo wake kufuati kuaawa kwa George Floyd na afisa wa jeshi la Polisi.

Kifo cha Floyd  kwa kukandamizwa  ni kitendo kinachostahili kukemewa, kitendo hicho kimetokea  Minneapolis Marekani kinaskitisha mno, kifo hicho kimepelekea maandamano  licha ya  harakati za usawa wa haki kwa kipindi cha miaka mingi.

Katika ujumbe wake   huo  rais Erdoğan amekumbusha ujumbe wa  uislamu katika utamduni wake na maagizo kutoka kwa mwenyezi mungu kuwa binadamu anahimizwa  kuheshimu  nafsi ya binadamu na kiumbe chochote kile na Uturuki  kila siku itaendelea  kupinga ukiukwaji wa haki .

Hakuna   mtu  aliebora kuliko mwingine, mweusi sio bora mbele ya mzungu na mzungu sio bora kuliko mweusi ameendelea kusema rais Erdoğan.

George Floyd amefariki baada ya kukamandamizwa na goti na afisa wa jeshi la jeshi la Polisi , kitendo  hicho  kimerikodiwa kwa kutumia simu  ya mkononi na kurushwa moja kwa moja  katika   ukurasa   mtandoa wa Facebook.

Tukio hilo limepelekea maandamano makubwa  Minneapolis na kusababisha uharibifu.

George Floyd amefariki akiwa na umri wa miaka  46.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items