Klabu ya hiyo ya Korea Kusini ilibidi iombe msamaha baada ya mashabiki kuwalaumu kwa kuwaweka wanasesele wa ngono katika nafasi za kukaa mashabiki.
FC Seoul ilisisitiza kuwa walikua ni "wanasesele wanaotumiwa katika kuuza nguo madukani" na wala sio wanasesele wa ngono -lakini ikakiri kuwa waliwapata kutoka katika kampuni inayotengeneza wanasesele wa ngono.
Na baadhi ya wanasesele walikua wakionyesha ishara za wavuti wa matangazo ya ngono-licha ya kwamba ponografia imepigwa marufuku nchini Korea Kusini.
Ni nini kilichotokea katika mechi ?
JUmapili, FC Seoul ilicheza mchezo wao wa kwaza ya msimu wa Ligi ya Korea Kusini - League K
Uwanja ulikua mtupu- ikiwa ni moja ya hatua zilizochukuliwa kuzuwia mlipuko wa Covid-19.
Kwa hiyo kabla ya mechi, kampuni inayoitwa Dalcom ilijitolea kujaza nafasi za viti zilizoachwa wazi, na klabu ikakubali. Kwa ujumla, walikua ni wanasesele 30- 25 kati yao walikua ni wanawake na watano walikua ni wanaume.
Hatahivyo, mashabiki waliokua wakitazama mechi hiyo kwa njia ya mtandao walibaini kuwa baadhi ya wanasesele waliokua na muonekano kama wa wanasesele wa ngono -jambo lililoilazimisha klabu iombe radhi kupitia kurasa zake za Facebook na Instagram.
Klabu ya FC Seoul ni mojawapo klabu zenye mafanikio makubwa nchini Korea Kusini-picha hii inaonyesha mashabiki wakati wa mechi ya Championi Ligi ya Asia mwezi Februari
Afisa wa klabu hiyo Lee Ji-hoonameiambia BBC kuwa haikufanya uchunguzi juu ya kampuni ya Dalcom, na haikufahamu kazi inayofanya.
Lakini klabu hiyo imesema kwamba Dalcom ilisisitiza kuwa wanasesele inaowapatia ni "wale wa kawaida wanaotumiwa kuuza nguo madukani ", na wala hawahusiani kabisa na ponografia.
Bwana Lee amekiri kuwa alihisi kwel;i wanasese hao "walionekana swa kabisa na binadamu " - lakini akasema haikumuingia akilini kwamba wangekua ni wanasesele wa ngono.
Mechi za soka zilifufuliwa lini Korea Kusini?
Msimu wa 2020 wa K League ulitakiwa kuazna mnamo mwezi wa February lakini ulicheleweshwa kutokana ana mlipuko wa virusi vya corona
Lakini mafanikio ya Korea Kusini katika mapambano dhidi ya virusi yaliruhusu kufufuliwa kwa soka mapema kuliko maerneo menginge duniani.
Na, wakati msimu ulipoanza tarehe 8 Mei, K League yalikua ni mojawapo ya maeneo muhimu kwa mashabiki wa kuelekeza macho yao- jambo lililofanya dunia kufuatilia mechi zao.
