Klabu ya Simba na Mo Dewji kugawa barakoa 25,000 Dar

Klabu ya soka ya Simba kwa kushirikiana na mwenyekiti wake Mohamedi Dewji Mo kupitia taasisi ya Mo Dewji Foundation leo wameamua kugawa barakoa kwa wakazi wa  Dar es Salaam ili kupambana na janga la ugonjwa wa corona.

Barakoa hizo zitagaiwa bure siku ya leo katika maeneo mbali mbali ya jiji la Dar es Salam ususani Kivukoni, kariakoo, buguruni, Temeke pamoja na Mbagala


Kupitia ukurasa wa instagram Mo Dewji ameandika;

"Katika kupambana na janga la ugonjwa wa corona, kuanzia leo nimeamua kugawa barakoa 25,000 BURE kwa Watanzania wenzangu kupitia taasisi ya @DewjiFoundation kwa kushirikiana na timu yetu ya @SimbaSCTanzania Tuzitumie vizuri ili tujilinde na #COVID1





Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items