Mtatiro avunja ndoa ya wanafunzi wa darasa la saba

Mkuu wa Wilaya ya Tunduru,Ruvuma, Julius Mtatiro  ameendeleza oparesheni ya kuwafuatilia Watoto walioko majumbani wakati huu wa likizo ya corona na kubaini Watoto wawili wakiwa wanaishi kama Mke na Mume, Watoto hao wanasoma darasa la saba katika Shule ya Msingi Mchangani, Tunduru.

Mtatiro amekutana na Wazazi wa Watoto hao pamoja na Watoto wenyewe na ametoa adhabu ya viboko kwa Mtoto wa kiume na kumnyoa nywele hadharani pamoja na hatua nyingine za kisheria ikiwemo kuendelea kumshikilia.

DC Mtatiro ameelekeza Wazazi wa Watoto hao washitakiwe kwasababu kuna ushahidi wa wazi kuwa walikula njama na kuwaruhusu Watoto waishi kinyumba na hata kuwapangishia nyumba ambayo wameendelea kuishi kama Mke na Mume wakati huu ambapo shule zimefungwa.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items