Mvua na ukuta wa nyumba vyaua watu 11 Morogoro

Watu 11 wameripotiwa kupoteza maisha katika matukio mawili tofauti ikiwemo watoto 7 kusombwa na maji wilayani Mvomero na huku watu wengine wanne wa familia moja kuangukiwa na ukuta wakiwa wamelala.

Akithibitisha kutokea kwa matukio hayo, Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa amesema kuwa tukio la kwanza  watu wanne wa familia moja wamefariki dunia baada ya kuangukiwa na ukuta usiki wa kuamkia Mei 15 katika nyumba waliyokuwa wakiishi katika kijiji cha Konde, Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro.

Kamanda mtafungwa amewataja waliopoteza maisha ni Godfrey Agustino (35), Joyce Claud (38), mariana Godfraya (10), Senarino Godfrey (5).

Katika tukio lingine, watu 7 akiwemo mtoto mchanga wamefariki dunia baada ya kusombwa na maji kufuatia mvua kubwa iliyonyesha maeneo ya milimani na kusababisha maji mengi kuingia kwenye makazi ya watu wakiwa wamelala.

Mwili wa mtoto ambaye alikuwa amezaliwa siku chache zilizopita haujapatikana na juhudi za kuutafuta bado zinaendelea.