RC Zambi aitaka halmashauri ya Ruangwa iweke kipaumbele mpango wa matumizi bora ya ardhi

 Na Ahmad Mmow, Lindi.

Mkuu wa mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi ameitaka halmashauri ya wilaya ya Ruangwa iweke kipaumbele mpango wa matumizi bora ya ardhi katika vijiji vilivyopo kwenye halmashauri hiyo.

Zambi alitoa agizo hilo jana mjini Ruangwa, wakati wa kikao cha baraza maalumu la madiwani kwa ajili ya kupokea taarifa ya ukaguzi    ya mkaguzi na mthibiti wa hesababu za serikali  katika halmashauri hiyo.

Zambi alisema unatakiwa mpango wa matumizi bora ya ardhi wenye ufanisi na matokeo mazuri na vijiji vingi vipimwe. Kwani ni jambo muhimu kufanyika.

Zambi ambaye alitoa agizo hilo kutokana kutoridhishwa na idadi ndogo ya vijiji vilivyopimwa na kuingia kwenye mpango wa matumizi bora ya ardhi, alisema nijambo lisilokubalika kuona vijiji vingi havijaingia kwenye mpango huo muhimu. Kwani unanafasi kubwa ya kupunguza migogoro ya ardhi.

Kufuatia kutoridhishwa na kasi ya upimaji aliitaka iweke kipaumbele kwa kutenga fedha zitakazo tumika kwa ajili ya upimaji.

" Kuwe na mpango maalum wa matumizi bora ya ardhi. Sio  mnapima vijiji viwili, vitatu halafu basi. Vijiji 17 kati vijiji 90 ni vichache sana," alisisitiza Zambi.

Mbali na agizo hilo mkuu huyo wa mkoa wa Lindi aliitaka halmashauri hiyo ihakikishe fedha ambazo zimekopeshwa kwa vikundi vya ujasiriamali ambazo hazijareshwa, zirejeshwe. Kwani  bado inatakiwa kuendelelea kutoa mikopo ya fedha zinazotokana na mapato yake ya ndani.

Alisema kunauwezekano kwamba baadhi ya vikundi vilivyokopeshwa vimekufa. Hata hivyo haiwezi kuwa sababu ya kutorejesha mikopo iliyokopa.  Kwani waliokopesha wanawajua waliowakopesha nanilazima zilipwe.

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items