Rais wa Uturuki Recep Tayyip ErdoÄŸan amefanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Iraq Mustafa al Kadhimi.
Kulingana na taarifa kutoka ikulu ya rais mjini Ankara,viongozi hao wawili wamefanya mazungumzo ya simu.
Katika amzungumzo hayo rais ErdoÄŸan ametoa pongezi kwa waziri huyo na kumtakia mafanikio katika wadhfa wake.
Viongozi hao wawili pia waligusia mada tofauti kama vile mbinu mbalimbali za kupambana na virusi vya corona na vilevile masuala ya kanda.
Uturuki na Iraq zimeonyesha kuwa na uhusiano mzuri.
