Nigeria imewauwa wanachama 61 wa Boko Haram Kaskazinimashariki mwa nchi hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari, John Enenche, msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Nigeria, amesema jeshi la nchi hiyo linaendeleza mashambulizi dhidi ya Boko Haram katika jimbo la Adamawa.
Enenche amesema magaidi 61 wa Boko Haram waliuawa na wengi walijeruhiwa wakati wa mashambulizi hayo.
Magaidi wengi wamejisalimisha na silaha zao kukamatwa.
Msemaji huyo amesema jumla ya magaidi 603 wamejisalimisha kwa serikali tangu mwanzoni mwa mwaka.
Zaidi ya watu 30,000 wameuawa na karibu milioni 3 wamekimbilia makazi yao katika muongo mmoja wa mashambulizi ya kigaidi ya Boko Haram nchini Nigeria, kulingana na Ofisi ya UN ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu.
Vurugu zinazofanywa na Boko Haram zimeathiri watu wapatao milioni 26 katika eneo la Ziwa Chad na kuwahamisha wengine milioni 2.6, kulingana na Chombo cha Wakimbizi cha UN.
