Rais wa Marekani Donald Trump amesema ametoa ruhusa ya kutengenezwa kwa kombora jipya lenye teknolojia ya kisasa la hypersonic, ambalo litakuwa lina kasi kubwa zaidi kuliko kombora lolote linalomilikiwa na Urusi pamoja na China.
Trump amesema amelipa kombora hilo jina la, "super,duper", na kwamba amearifiwa kuwa litakuwa na kasi mara 17 zaidi kuliko makombora yanayomilikiwa na mahasimu wake.
Hivi karibuni Urusi ilitangaza kuwa imezindua kombora lenye uwezo wa kubeba mzigo wa nyuklia unaosafiri kwa kasi kubwa.
Rais wa Urusi Vladimir Putin alisema kombora hilo la Avangard hypersonic lilianza kufanya kazi mnamo mwezi Desemba.
China nayo pia imekuwa ikitengeneza kombora la hypersonic lakini kasi yake haizidi ile ya kombora la Urusi, ingawa ni la teknolojia ya kisasa zaidi kuliko makombora yanayomilikiwa na Marekani.
