Tetesi za soka leo jumatano



Newcastle imeanza mazungumzo ya kumsajili kiungo wa kati wa Barcelona Philippe Coutinho, 28, baada ya Bayern Munich kubadili nia ya kumpatia mkataba wa kudumu nyota huyo wa kimataifa wa Brazil. (Mundo Deportivo - in Spanish)

Magpies pia wanamlenga kiungo wa kati wa Liverpool Xherdan Shaqiri, 28, dirisha la uhamisho wa wachezaji litakapofunguli tena msimu wa joto. Kiungo huyo wa kimataifa wa Uswizi amewakilisha klabu hiyo mara 10 tu msimu huu. (Mail)


Arsenal na Tottenham wanang'ang'ania kumsajili kwa mkataba wa bila malipo kiungo wa kati wa Chelsea na Brazil Willian, 31, ambaye mkataba wake Stamford Bridge unakamilika msimu huu. (Telegraph)

Wolves huenda wakamnunua kiungo wa kati wa Sporting Lisbon Joao Palhinha, 24. (Mirror)


Manchester City wanaongoza katika kinyang'anyiro cha kumsaka kinda wa Ajax Sontje Hansen, 18, ambay alishinda tuzo ya Golden Boot katika kipute cha kombe la dunia kwa wachezaji walio na umri wa chini ya miaka 17 msimu uliopita. (Goal)

Klabu ya Portugal ya Vitoria Guimaraes inataka kumnunua mchezaji kinda wa Crystal Palace Jadan Raymond, 16, kwa £250,000 kandarasi yake ikielekea kumalizika mwisho wa mwezi ujao. (Sky Sports)

Everton imewasilisha ombi la £40m kumsaini kiungo wa kati wa Napoli, Allan, 29, lakini klabu hiyo inataka dau la £60m kumuuza raia huyo wa Brazil. (Il Mattino - in Italian)


The Toffees pia wamewasilisha ombi la $25m kwa Barcelona kumnunua beki wa Ufaransa Jean -Claire Todibo ,20, ambaye kwa sasa anahudumu kwa mkopo katika klabu ya Schalke nchini Ujerumani. (Mail)

Mshambuliaji wa Inter Milan na Argentina Mauro Icardi, 27, anakaribia kuhamia katika klabu ya Paris St-Germain kwa dau la £54m. (ESPN)


Paris St-Germain inafanya mazungumzo na Arsenal katika jaribio la kumsaini mashambuliaji wa klabu hiyo Pierre-Emerick Aubameyang, 30, kwa£34m. (Todofichajes)