Uturuki yaendelea kutoa msaada wa kupambana na Covid-19

Shirika la kutoa misaada katika  makito ya dharura la Uturuki TİKA   na ushirikiano wa kimataifa limetoa msaada wa  vifaa vya matibabu  nchini Afghanistani  katika jitihada za kupamba na virusi vya corona nchini Afghanistani.

Makama wa waziri wa afya wa Afghanistani Walid Mejruh  amefahamisha kuwa amepokea msaada wa vifaa vya matibabu kutoka Uturuki kwa moyo mkunjufu  kwa kuwa Uturuki imeikumbuka Afghanistani katika kipindi  hiki kigumu cha kupambana na maaambukizi ya virusi vya corona.

Katika hafla ya kukabidhi msaada huo,  Walid  amempongeza  mratibu wa TİKA Zühtü Çal  ambae ameonekana pia kuwa  mwenye furaha kwa  mapokezi .

Vifaa  vilivyotolewa ni pamoja  na  vifaa vya kupumlia na vifaa vingine muhimu katika vituo vya afya na hospitali.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items