Wafanyabiashara walalamikia uchafu wa mazingira soko la Makorora jijini Tanga



Na Rebeca Duwe, Tanga.

Baadhi ya wafanyabiashara wa soko la Makorora jijini Tanga wamelalamikia  hali ya uchafu wa Soko hilo hususan kipindi hiki cha msimu wa mvua  zinazoendelea kunyesha kwani wengi wamekuwa wakifanya biashara juu ya matope kutokana na miundo mbinu kutokuwa ya kuridhisha.

Wakizungumza  mapema leo kuhusu kero hiyo wafanyabiasha hao wamesema kwamba hali ya uchafu imekuwa ya siku nyingi kwani hata kama usafi ukifanyika lakini maji ya mvua yanakusanyika na kusababisha matope ambayo yanakaa kwa muda mrefu bila kukauka hali ambayo ni hatari kwa afaya za wananchi.


Aidha wameiomba serikali iweze kuwasaidia wafanyabiashara hao kwa kutengenezea miundo mbinu ikiwemo kumwaga zege ambayo itasaidia kupunguza matepo kukusanyika mahali pamoja na badala yake  wafanya watapa afueni tofauti na hali ilivyo kwa sasa.

Kwa upande wake mdau wa soko hilo Athumani Bakari amesema kero yake ni watendaji wadogo wa kata ya makorora kushindwa kusimamia utaratibu wa usafi tofutti na miaka kumi iliyopita kwani soko kwa sasa limekuwa chafu  jambo ambalo linahatarisha maisha ya wateja pamoja na wafanyabiashara.


Amesema kuwa viongozi wa serikali ya  ngazi ya juu kuweza kuingilia kati ili kuweza kuwasaidia wakazi wa jiji la Tanga kufanya  kuendelea kufanyabishara sokoni hapo kwani kwa sasa mazingira yaliyopo hayafai kuuzia biashara ya  vyakula  kama wanavyoendelea kuuza wafanyabiashara hao.

Naye Mgaza Amiri ambaye Mwenyekiti wa soko la Makorora amesema kwamba hali iliyopo hairidhishi  kwani tatizo kubwa ni kutokuwa mfereji wa kupitishia maji ili yasituame katika maeneo ya kufanyia biashara badala yake injinia wa jiji hajaweza kutoa mwongozo nini kifanyike .


Amesema yeye kama  mwenyeketi ameshaandika tayari kuwafikisha viongozi  wa serikali ya halmashauri ya jiji na kwamba bibi afya analijua hilo na kushuhudia mwenyewe hali ilivyo katika soko hilo.

 Sambamba na hayo ameiomba serikali kuwajengea  wafanyabiashara wa ndizi kwani kwasasa hawana sehemu ya kuhifadhiwa ndizi kwani kutokuwa na jengo la kuhifadhi na kuuzia ndizi ndio inayosababisha kujaa kwa matope sokoni hapo.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items