NA Timothy Itembe Mara.
Watu
watatu wanaosadikiwa kuwa wamachama wa Chama cha Demokorasia na
maendeleo Chadema wamekamatwa na jeshi la Polisi wilayani Tarime kwa
makosa ya kuvamia eneo lililokuwa limeandaliwa na Chama cha NCCR Mageuzi
kwaajili ya kuongea na vyombo vya habari juzi.
Akiongelea
kukamatwa kwa watuhumiwa hao mkuu wa wilaya Tarime,Mtemi Msafiri
alisema kuwa watu watatu wanaosadikiwa kuwa wafuasi wa Chama cha
Demokorasiaa na maendeleo Chadema wamekamatwa na jeshi la polisi kwa
kuwafanyia fujo na kuwaruishia mawe wanachama wa Chama cha NCCR Mageuzi
mahali ambao walikuwa wameandaa kuongea na vyombo vya habari juzi.
Msafiri
alikema kitendo hicho ambapo alisema kuwa jeshi la polisi
linawashikilia wafuasi wa Chadema watatu huku likiwahoji na upelelezi
ukikamilika watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani ili kujibu mashitaka
ya tuhuma ambayo yanawakabili.
Pia
mkuu wa wilaya hiyo aliongeza kusema kuwa wale wote waliohusika katika
kitendo cha kufanya fujo wataendelea kusakwa mahali popote walipo hadi
hapo watakapokamatwa na kufikishwa kwenye mkono wa sheria ili
kukabilioana na tuhuma zinazowakabili.
"Nimesikitishwa
sana na kitendo cha wafuasi wa Chama cha Demokorasia na maendeleo
Chadema kwenda na kuwafanyia fujo huku wakiwarushia mawe wanachama wa
Chama cha NCCR Mageuzi kwenye eneo walilokuwa wametenga kuongea na
vyombo vya habari kitendo hicho hakikubaliki ni kkinyume cha sheria
tutawasaka mahali popote walipo ili tuhakikishe tunawakamata na
kuwafikisha sehemu husika wale wote waliohusika"alisema Msafiri.
Mkuu
wa wilaya hiyo alimaliza kwa kusema kuwa Tarime sio kisiwa cha matukio
yasiyokubalika kisheria bali ni wilaya yenye kuishi kwa kuzingatia
sheria za nchi zilizopo na kuwa haiingii akilini watu kuishi kwa
kujichukulia sheria mkononi na kama Mtu au chama kimekwazwa kwa namna
yeyote kunahaja ya kulalamika sio vinginevyo.
