Watu 120 wameripotia kukamatwa Hong Kong katika maandamano ambayo yameanza upya baada ya kuonekana kuwa janga la virusi vya corona sio tena tishio katika jamii.
Waandamanajji wamemiminika mabarabarani kupinga mpango wa sheria mpya kutoka China ambayo inadiwa kuingilia masuala ya ndani ya Hong Kong.
Katika maandamano hayo, waandamanaji zaidi ya 120 wameripotiwa kukamatwa.
Mamia ya waandamanaji wamekusanyika mjini kati Causeway Bay wakiwa wamevalia mavasi meusi kama ishara ya kupinga msuada huo wa sheria.
Waandamanaji wamesikika wakitoa matamshi dhidi ya serikali.
Jeshi la kutuliza ghasia lmetumia mabomu ya kusababisha kutokwa na machozi kuwatawanya waandamanaji hao.
Miongoni mwa watu waliokamatwa, amekamatwa piia mwanaharakati maarufu anaefahamika kwa jina la Tam Kakchi.
Askari polisi wanne pia wameripotiwa kujeruhiwa katika maandamano hayo.