Waziri castiko aitaka bodi ya mfuko wa uwezeshaji kufanya kazi kwa uwaminifu


Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wazee Wanawake na Watoto Dk  Moudline Cyrus  Castico ameitaka Bodi  ya Mfuko  wa Uwezeshaji Wananchi Ki uchumi  kufanyakazi zake kwa ushirikiano, uaminifu na kujituma ili Mfuko huo uwe endelevu .

Hayo ameyaeleza wakati akizindua Bodi hiyo huko kwenye ukumbi wa
Wizara  yake Mwanakwerekwe wilaya ya Magharib  B’ Unguja.

Amesema kwa kufanya hivyo Mfuko huo utafikia  malengo
yake  na kutoa huduma za Mikopo kwa Wajasiriamali na Wananchi kwa ujumla.

Dr. Moudline amesema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imeanzisha
Mfuko huo ilii Wananchi wake wakopeshwe  ili kutunisha fedha za miradi yao
wanayoiendesha  ili kuweza kujiajiri na kujipunguzia umaskini.

“Mahitaji yamekua makubwa maombi ya Mikopo yanapokelewa kila siku
,hivyo mshirikiane na Uongozi  wa Wizara ili kupata mbinu za pamoja za
kutunisha fedha kupitia Mfuko huo “Ameisisitiza bodi hiyo .

Halkadhalika ameitaka Bodi kujenga tabia ya kutembelea wateja wa
Mfuko huo waliopo Mjini na Vijijini  Unguja na Pemba ili  kuona
maendeleo yao katika miradi mbalimbali  wanayoiendesha pamoja na
kuhamasisha wananchi kutumia huduma za Mfuko huo.

Bodi hiyo ambayo ina wajimbe  Sita  Mwenyekiti wake
ni  Bi.Amina Ismail  Kanduru  na wajumbe ni Bw. Ali Aboud Mzee ,
Bi.Fatma Iddi Ali, MHE. Ahmada Yahya Abdulwakil , Bw. Suleiman Haji
Ali  Bi. Mwanahija Almasi  Ali . na Bi. Abeida Rashid
Abdalla.     

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items