Halmashauri ya Rorya yapunguza vifo vya kina mama na watoto kwa mwaka



Na Timothy Itembe Mara.

HALMASHAURI ya Rorya mkoani Mara imepunguza vifo vya mama na mtoto kutoka 15  kwa 100  vya kina mama huku vifo vya watoto vikipungua kutoka 02  kwa 100 hadi 01 kwa kila mwaka.

Hayo yalibainishwa jana na Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Rorya,Charles Chacha mbele ya mgeni,mkuu wa wilaya Tarime,Mtemi Msafiri aliyehudhuria sherehe za uzinduzi wa hospitali ya wilaya kwa niaba ya mkuu wa mikoa Mara,Adam Kigoma Malima.

Chacha alisema kuwa kwa sasa  Halmashauri ya Rorya imepunguza vifo vya kina mama na Mtoto katika halmashauri hiyo kwa mwaka na kuwa Hospitali inayoenda kuzinduliwa itasaidia kupunguza vifo hivyo kama sio kumaliza tatizo hili kwa ujumla.

Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Rorya,Lameck Airo alisema kuwa ujenzi wa hospitali hiyo umefanikiwa kutokana na Ombi maalumu alilotoa kwa Rais,John Pombe Magufli wakati wa ziara yake mkoani Mara akiwa wilayani  Tarime la kuwapatia fedha kwa ajili ya ujenzi wa Hoapitali na Rais kuridhia na kuwapatia shilingi Bilion 1.5.

Airo alitumia nafasi hiyo kuwataka wananchi na wakazi wa Rorya kupenda shuguli za maendeleo kwani serikali itakuwa inatoa fedha pale ambapo wananchi wanania ya kuchangia shuguli za maendeleo.

Mbunge huyo aliongeza kuwataka wananchi wa Rorya kutegesha katika ujenzi wa Maboma ili kupata fedha za serikali kwa lengo la kukamilishia ujenzi kwa kuzingatia kuwa hiyo ndiyo Sera ya serikali kuwa wananchi waanze kujenga maboma serikali imelizie kupaua.

Katika halfa hiyo mgeni Rasimi ambaye ni mkuuwa wilaya Tarime alimtaka Diwani kata ya Kitembe kupitia chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema,Thomas Patirrick Rissa  kusema neon la kujiuzuli Chama chake na kuhamia Chama Tawala cha CCM ambapo diwani huyo aligoma na kutumia nafasi hiyo kuomba upinzani kuwepo kwani ni haki ya kikatiba na serikali bila upinzani nisawa na kupika makande bila Maharage. 

Mkuu wa wilaya Tarime,Mtemi Msafiri  kwa niaba ya mgeni rasimi mkuu wa mkoa Mara,Adam Kigoma Malima aliyekuwa amealikwa kuhudhuria uzinduzi huo alichukua nafasi hiyo kwa kumshukuru Rais awamu ya Tano,John Pombe Magufuli kwa kutoa fedha za ujenzi wa hospitali 67 Nchi nzima na Hospitali ya  Rorya ikiwemo hiyo ikiwa ni kujali Afya za Watanzania.

Msafiri aliwataka wananchi wa Rorya pamoja na watendaji  wa halmashauri hiyo kuendelea kuitunza hospitali hiyo ili idumu na kutimiza kwa lengo la kutimiza malengo yaliyokusudiwa.

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items