Marekani kuwawekea vikwazo maafisa wa China wanaokandamiza demokrasia Hong Kong

Waziri wa Mambo ya kigeni wa Marekani Mike Pompeo amesema serikali mjini Washington itawapiga marufuku ya kuingia Marekani maafisa kadhaa wa China wanaohusika na kuminya demokrasia mjini Hong Kong.

Bila kutaja majina ya maafisa hao wa China, Pompeo amesema vikwazo vya kuingia Marekani vitawekwa kwa viongozi wa sasa na wa zamani wa chama cha kikomunisti cha China wanaoaminika kuwa wanahusika na kutishia hadhi na uhuru wa mji wa Hong Kong.

Hatua hiyo inakuja kuelekea mkutano wa siku tatu wa bunge la China unaoanza siku ya Jumapili na ambao unatarajiwa kutunga sheria mpya ya usalama wa taifa kwa ajili ya Hongkong ambayo tayari imezusha ukosoaji kutoka mataifa ya kigeni na wanaharakati wa demokrasia.

Tangazo la Pompeo ni hatua ya kwanza madhubuti kuchukuliwa na Marekani dhidi ya mipango ya China ya kutunga sheria mpya ya usalama lakini wachambuzi wa masuala ya siasa wamesema vikwazo hivyo ni ishara isiyo na uzito mkubwa.

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items