Misri, Ethiopia na Sudan zimefikia makubaliano ya kusitisha kwa muda mpango wa kulijaza maji bwawa kubwa la kufua umeme la Ethiopia kama sehemu ya mkataba mpana kuhusu mradi huo ambao umechochea mvutano kati ya mataifa hayo matatu.
Ofisi ya rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi imesema jana kuwa makubaliano hayo yaliyo na nguvu kisheria yanazuia pande zote dhidi ya kuchukua hatua bila kushirikisha upande mwingine ikiwemo uamuzi wa kujaza maji katika bwawa la kufua umeme la Renaissance.
Hapo kabla Ethiopia ilitangaza mipango ya kuanza kujaza maji katika bwawa hilo kubwa ndani ya mto Nile kuanzia mwezi unaokuja, licha ya upinzani mkali kutoka Misri na Sudan ambazo ziliwasilisha malamiko yake mbele ya Umoja wa mataifa wiki iliyopita.
Ujenzi wa bwawa hilo ambalo Ethiopia inasema ni muhimu katika kuongeza uzalishaji wake wa nishati ya umeme umezusha msuguano kati ya nchi hiyo na Misri inayozingatia mradi huo kuwa kitisho kwa upatikanaji wa maji ya mto Nile inayoategemea kwa karibu asilimia 97.