TAASISI inayopambana na matumizi ya Dawa za kulevya wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani (MEFADA), katika kipindi cha miezi mitano imewafikia wahanga wa matumizi ya dawa hizo wapatao 195.
Kati ya wahanga hao 68 wanaendelea na matibabu ya dawa ya Methadone, inayosaidia kumkomboa mtumiaji ambapo wengi walioachana walianza kwa matumizi hayo, hatimae kuachana kabisa na kuwa kati yao ndio wanaoshiriki utoaji wa elimu kwenye taasisi hiyo.
Hayo yamebainishwa na Mratibu wa mpango huo wilayani hapa Bedinego Makoye, akizungumza na Waandishi wa habari ambapo alisema taasisi inahudumia Vijiji na Vitongoji vinavyounda Kata 11, washirikiana na Wenyeviti wa Serikali, Watendaji, wakiwemo walioacha ambao kati yao ndio wanaoitumikia taasisi hiyo.
Alisema kuwa ofisi yao iliyopo Kata ya Magomeni wilayani hapa, inafanya shughuli hizo chini ya ufadhili wa Serikali kupitia Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, ambayo iliyoanza mwaka 2014 kisha kusajiliwa 2015, chini ya sheria ya Serikali namba 24 ya mwaka 2002.
"Awali tulikuwa tunakuja Bagamoyo tunafanyakazi kisha tunaondoka, lakini mwezi wa pili mwaka huu 2020 tukafanikiwa kuipata hii ofisi ambayo tumepanga, na kwa kipindi hicho tumeweza kuwafikia vijana 195 waliokuwa wahanga wa dawa, wengine tunao tunafanyakazi pamoja," alisema Makoye.
Kwa upande wake Magreth Noni ambaye ni mwalimu wa wahanga hao, alisema kuwa yeye ni mmoja wa waliokuwa wanatumia dawa za Kulevya, ambae alijikuta amejiingiza mwaka wa 2004/2005 akiwa Visiwani Zanzibar kabla ya kuacha mwaka 2015.
Alisema kwamba sababu kubwa zinazochangia vijana waliowengi kujiingiza katika matumizi hayo ni makundi lika, ambapo asiyetumia anapojiunga na wanaotumia nae anajikuta anajiunga anaingia katika mtego pasipokutarajia, hatua inayotokana na ushawishi.
Aliongeza kuwa yeye alishawishiwa na rafiki yake wa kiume mzungu, ambaye alimweleza kuwa atapotumia dawa atakuwa na hisia kali katika mahusiano ya kimapenzi, hivyo akajikuta anaingia katika mtego huo wakati huo akiwa Visiwani Zanzibar.
"Nikiwa Visiwani Zanzibar nilikutana na rafiki wa kiume wa Kizungu aliyenishawishi, kwa madai kuwa inaongeza hisia za mapenzi nikajikuta natumia, ilikuwa mwishoni mwa mwaka 2004/2005, kabla ya kuacha mwaka 2015, hivi sasa ni mwalimu yewaelimisha walioathirika," alimalia Magreth.