Netanyahu ataka kurejeshwa vikwazo vikali dhidi ya Iran

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netayahu leo ameyatolewa wito madola yenye nguvu duniani kurejesha vikwazo vikali dhidi ya Iran huku akiahidi kupunguza kile alichokiita ´´uchokozi´´ wa Tehran kwenye kanda ya mashiriki ya kati.

Netanyahu ameliambia Baraza lake la Mawaziri kuwa shirika la umoja wa mataifa la nguvu za atomiki IAEA limebaini kwamba Iran ilikataa wataalamu wa shirika hilo kutembelea vituo vya siri ambavyo inashuku huvitumika kuendelesha shughuli za nyuklia.

Shirika hilo lilisema siku ya Ijumaa, kuwa Iran ina hifadhi madini ya urani yaliyorutubishwa mara nane zaidi ya ukomo uliowekwa na mkataba wa kupunguza shughuli zake za nyuklia wa 2015 kati ya nchi hiyo na mataifa yenye nguvu.

Netanyahu ameyataka mataifa mengine duniani kujiunga na Marekani kwa kurejesha vikwazo dhidi ya dola hiyo ya kiislam akiituhumu Iran kukiuka ahadi ilizotoa kwa kuficha vituo vya nyuklia pamoja kurutubisha madini ya urani
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items