Serikali ya Uingereza imesema leo itaruhusu kufunguliwa tena kwa nyumba za ibada kwa mtu mmoja mmoja ifikapo Juni 15 wakati taifa hilo likijaribu kuharakisha kuondoa vizuziizi vya viruis vya corona ili kunusuru ajira.
Ofisi ya wazrii mkuu Boris Johnson imesema ibada za makundi na mikusanyiko mengine ya kidini itaendelea kupigwa marufuu kutokana na wasiwasi kwamba virusi vya corona vinasambaa haraka kwenye maeneo yasiyo na uwazi.
Uingereza inalenga pia kufungua tena maduka ifikapo Juni 15 katika juhudi zake za kurejesha maisha ya kawaida tangu ilipoweka marufuku kali kuzuia kuenea virusi vya corona Machi 23. Tayari idadi ya watu waliokufa na ugonjwa wa COVID-19 nchini Uingereza imefikia 40,400 ikiwa nchi ya pili kwa idadi kubwa ya vifo duniani baada ya Marekani.