Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis leo Jumapili amewahimiza Waitaliano kuendelea kujilinda dhidi ya maambukizi ya virusi vya corona licha ya viwango vya maambukizi kupungua nchini Italia.
Papa Francis, ameyasema hayo alipowahutubia mamia ya waumini katika uwanja wa mtakatifu Petro mjini Vatican walikusanyika kuhudhuria ibada ya misa ya Jumapili.
Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki amesema licha ya idadi ya waliohudhuria misa ya leo kuwa ndogo lakini ni ishara kwamba Italia imesimama tena baada ya kukabiliwa na hali mbaya ya ugonjwa wa COVID - 19.
Amewasihi watu kuendelea kutii amri zilizowekwa na serikali za kuzingatia kukaa kwa umbali unaoshauriwa na kuvaa barakoa ili kupunguza maambukizi ya corona. Karibu watu 34,000 wamekufa nchini Italia na kuifanya nchi hiyo kuwa ya nne ulimwenguni kwa idadi kubwa ya vifo vya janga la corona baada ya Marekani, Uingereza na Brazil.