Wavuvi 7 Watanzania wawekwa karantini baada ya kuokolewa baharini Kenya

Wavuvi wa saba raia wa Tanzania waliookolewa baada ya boti yao kupinduka katika bahari ya hindi siku tatu zilizopita wamewekwa karantini katika kituo kilichopo katika kaunti ya Kilifi.

Wavuvi hao waliokolewa na maafisa polisi pwani ya Kenya baada ya kuhitaji msaada baada ya chombo chao kupata tatizo la kiufundi.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation nchini Kenya, Mkurugenzi wa mamlaka ya maji (KMA) George Okong'o amesema wavuvi hao waliokuwa kwenye chombo hicho cha majini kwa jina la FV Haina Hollo, kilichosajiliwa Tanzania walipelekwa katika kituo cha katantini cha Kilifi.

''Boti hiyo ilitoka Tanga kuelekea Pemba tarehe 2 mwezi Juni ikiwa na miche 700 ya mkaratusi kabla ya chombo hicho kukumbana na upepo mkali, na kusombwa maji baada na kupoteza uelekeo. Hali ya chombo hicho kupoteza ulekeo kutokana na upepo mkali ndicho kinachodhaniwa kusababisha chombo hicho kuingia kwenye maji ya Kenya,'' alisema bwana Okong'o.

Amesema wavuvi hao walikuwa katika hali ya uchovu na wakiwa dhoofu.

Mamlaka ya KMA imejulisha mamlaka ya maji nchini Tanzania pia ubalozi wake mjini Mombasa kuhusu tukio hilo na pia wana mawasiliano na mmiliki wa chombo hicho cha majini. Tunawashauri wavuvi kuwa waangalifu na pia tumetoa waraja wa tahadhari kuhusu upepo mkali unaoshuhudiwa sasa katika bahari ya hindi wakati huu mpaka mwezi Agosti.'' alinukuliwa mkuu huyo wa TMA na gazeti la Daily Nation.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items