https://monetag.com/?ref_id=TTIb Polisi Korea Kusini wavamia ofisi ya mwanaharakati dhidi ya Kaskazini | Muungwana BLOG

Polisi Korea Kusini wavamia ofisi ya mwanaharakati dhidi ya Kaskazini

Jeshi la polisi nchini Korea Kusini leo limevamia ofisi ya mwanaharakati Park Sang- hak ambaye kampeini yake ya kurusha vijikaratasi vya ujumbe dhidi ya Korea Kaskazini imeongeza mvutano katika rasi ya Korea.

Polisi inasema kuwa maafisa wake walitembelea ofisi ya Park mjini Seoul kuchukuwa vijikaratasi hivyo, vitabu vya akaunti na vifaa vingine na kwamba Park atatakiwa kufika mbele yake kwa uchunguzi.

Park, mkimbizi wa Korea Kaskazini aliyeanzisha hatua ya kurusha mabofu yaliobeba vijikaratasi vya propaganda dhidi ya Korea Kaskazini kwa miaka mingi , amekuwa akiangaziwa baada ya Korea Kaskazini ghafla kuanza kutumia kampeini yake kama sababu ya kuhalalisha mfululizo wa hatua za uchokozi dhidi ya Kusini.

Wachambuzi wanasema hatua za Korea Kaskazini zinalenga kupata makubaliano ya nje inapokabiliwa na vikwazo vya Marekani na janga la virusi vya corona.